IMETOSHA KUSEMA UTAFANYA, ANZA LEO.

Imetosha sasa kusema kila siku utafanya, hebu anza leo kufanya.

Najua inaweza kuwa ngumu kwa sababu ya changamoto mbalimbali lakini hebu we anza tu kwa sababu kama hutafanya basi kwa hakika hakuna kitakachofanyika, anza leo.

IMETOSHA KILA SIKU KUSEMA UTAFANYA, ANZA LEO KUFANYA.

 

"Men of action are favored by the Goddess of good luck."

 — George S. Clason.

 

 

Rafiki yangu mpendwa, Moja ya tabia hatarishi sana na ambazo huwazuia watu wengi kufanikiwa basi hii tabia ya kughairisha mambo ni mojawapo.

 

Tangu mwaka jana umekuwa ukijiambia kwamba utaanza kufanya lakini mpaka hivi leo bado hujaanza kufanya yale uliyosema utafanya. Kisingizio kikubwa kwako ni kwamba eti unasubiria uwe tayari ndiyo ili uanze, rafiki yangu, "Utayari ni maamuzi, siyo hali." 

Hii ni kusema kwamba, Kama utaamua kuwa tayari hata hivi leo basi utakuwa tayari, hebu amua kuwa tayari ili uanze kufanya maana mwaka unaweza kuisha bila ya wewe kuanza. 

 

 Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka hapa ambapo dunia ipo leo, hakuna aliyefanikiwa kwa kusema tu bila kufanya. 

Miongoni mwa tofauti kubwa sana ya watu wanaofanikiwa na wale wasiofanikiwa ni hii, Watu wanaofanikiwa wao ni watu wa vitendo zaidi kuliko maneno, wao wakisema watafanya jambo fulani basi huweka sababu zote pembeni hivyo huhakikisha wanafanya jambo hilo. 

 

Watu wasiofanikiwa wao ni watu wa maneno zaidi kuliko vitendo, wao husema watafanya lakini wasifanye na huona sawa tu, wao huamini kwamba wanao muda mwingi sana hivyo watafanya tu. 

 

Hebu jiulize hapo ulipo, Hali ikoje kwako? Je! Wewe ni mtu wa vitendo au ni mtu wa maneno?

Kuwa mkweli kwako wewe mwenyewe maana ikiwa utajidanganya basi huwezi kubadilika, hivyo basi kama jibu litakuwa wewe ni mtu wa maneno kuliko vitendo basi amua leo kuwa mtu wa vitendo. 

 

George S. Clason katika kitabu chake cha "The Richest Man In Babylon" yaani "Tajiri Mkubwa Wa Babeli" anasema hivi, "Watu wa vitendo wanapendelewa na Mungu wa bahati njema."

 

Hii inatufundisha mambo muhimu yafuatayo;

 

Moja, Bahati huenda kwa watu wa vitendo na huwakimbia watu wa maneno. 

 

Mbili, Mungu hapendelei watu wa maneno bali watu wa vitendo. 

Hivyo basi ikiwa unataka Mungu akupendelee wewe pia, amua leo kuwa mtu wa vitendo. 

 

Tatu, Nenda kinyume na mazoea. 

Ukisema utafanya, muda ukifika weka sababu zote pembeni kisha fanya. 

 

Imetosha sasa kusema kila siku utafanya, hebu anza leo kufanya.

Najua inaweza kuwa ngumu kwa sababu ya changamoto mbalimbali lakini hebu we anza tu kwa sababu kama hutafanya basi kwa hakika hakuna kitakachofanyika, anza leo. 

 

Uwe na tafakari njema na siku njema pia.

 

Rafiki na Mwalimu wako, Yamungu Alinoti. 

 

Baada ya utambuzi, chukua hatua. 

 


Alinoti Espoir

25 Blog posts

Comments
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good

 
 
Adeline Nayituriki 2 yrs

Good